89 Flashcards
It’s height is 19,341 feet above the sea, and it is the highest mountain in Africa.
Urefu wake ni futi elfu kumi na tisa, Mia tatu, arobaini na moja juu ya bahari, pia ni mrefu kushinda milima yote Afrika.
You need about 5 days to climb this mountain, that I to say three days to climb up and 2 to come down.
Wahitaji kama siku tanu tanu kuupanda mlima huo, yaani siku tatu kupanda, na siku mbili kutelemka.
If you carry some of your loads, the journey will not be very expensive, perhaps one hundred shillings or more.
Ukichukua mizigo yako mingine safari haitakuwa ghali sana, labda, shilingi mia moja au zaidi.
But if you get hired porters to carry all your luggage, the journey will be More expensive.
Lakini ukiajiri wapagazi kuchukua mizigo yako yote, safari itakuwa ghali zaidi.
Also, you must hire a guide (who also needs a porter), because you would easily lose your way without a person to show you the path itself.
Pia, lazima uajiri mwongozi (anayehitaji mpagazi vilevile), kwa sababu ungepoteza njia yako kwa urahisi bila mtu wa kukuonyesha njia yenyewe.
Again, on the last day of climbing, people set off at about midnight, or 1am, so as to reach the summit at dawn.
Tena katika siku ya mwisho ya kupanda, watu huondoka kama saa Sita au Saba usiku ili wafike kileleni alfajiri.
There is a lot of cold up there at the top, so it is necessary to wear suitable clothes to prevent the cold from entering your body.
Kuna baridi nyingi sana kule juu, kwa hiyo (basi) ni lazima kuvaa nguo za kufaa kuzuia baridi isiingie mwilini mwako.
If you reach the summit, you will find a book for putting your name to show everybody that you have succeeded in climbing this great mountain.
Ukifika kileleni, utakuta kitabu cha kuandikia jina lako kuonyesha kila mtu kwamba umefaulu kupanda huo mlima mkuu.
When you reach the bottom part again, the porters give you a crown of flowers which grow on the slopes of the mountain.
Ufikapo sehemu ya chini tena, wapagazi wakupa taji ya maua yaotayo katika mitelemko ya mlima.
This crown shows that you have indeed conquered the highest mountain in Africa.
Taji hiyo yaonyesha kwamba wewe ndiye (ndiwe), umeshinda mlima mrefu kushinda yote Afrika.
Every visitor to Tanzania wants to climb this huge and beautiful mountain which is called Kilimanjaro.
Kila mgeni wa Tanzania hutaka kupanda mlima mkubwa na mzuri huu uitwao Kilimanjaro.