Edward Sep 15 Flashcards
I can go to America any month because I have time.
Ninaweza kuenda katika America mwezi wowote kwa sababu nina wakati.
Any year is good.
Mwaka wowote ni mzuri.
We will use any fruit to prepare fruit juice.
Tutatumia tunda lolote kutayarisha maji ya matunda.
We can use any car for carrying things.
Tunaweza kutumia gari lolote kubebea vitu.
Do you have any cold water for our guests?
Una maji baridi yoyote kwa wageni wetu?
Any news (plural) can be good if you can tell it well.
Habari zozote zinaweza kuwa nzuri unakiweza kuziambia vizuri.
Explain
Kueleza
Do you have any report about my patient?
Una ripoti yoyote kuhusu mgonjwa wangu?
We will use any road to go to the meeting.
Tutatumia barabara yoyote kuenda mkutanoni.
I will return home anytime.
Nitarudi nyumbani wakati wowote.
You can paint any wall.
Unaweza kupaka rangi ukuta wowote.
My wife uses any thread to knit a sweater.
Mke wangu anatumia uzi wowote kushonea sweta.
We will have the meeting anywhere in the hospital.
Tutakuwa na mkutano popote hospitalini.
If you walk anywhere in Kijabe you will not see a lion.
Ukitembea popote katika Kijabe, hutaona simba.
We can use any ball to play the game.
Tunaweza kutumia mpira wowote kucheza mchezo.
Do you have any bread?
Una mkate wowote?
All of the patients have already slept.
Wagonjwa wote wameshalala.
All people need to come on time to the meeting.
Watu wote wanahitaji waje kwa saa mkutanoni.
Do all doctors have a license to do this work?
Je, madaktari wote wana leseni kufanya kazi hii?
We will all be here and you all will be in the hospital.
Sisi sote tutakuwa hapa na nyinyi nyote mtakuwa hospitalini.
We will all be thankful if the meeting ends on time.
Sote tutashukuru mkutano ukikwisha kwa saa.
Children ate all of the food.
Watoto walikula chakula chote.
All of the dishes need to be washed.
Vyombo vyote vinahitaji vioshwe.
Oshwe passive -wa then subjunctive -we
All of the things came from Nairobi.
Vitu vyote vilitoka Nairobi.
All of the trees have a problem.
Miti yote ina shida.
The visitors are happy to eat the whole loaf of bread.
Wageni wanafurahi kula mkate wote.
The whole month did not have rain.
Mwezi wote haukuwa na mvua.
The whole car needs to be repaired.
Gari lote linahitaji lirekebishwe.
All of the milk has insects.
Maziwa yote yana wadudu.
All of the water will go to the hospital because it is important that hospital has water.
Maji yote yataenda hospitalini, kwa sababu ni muhimu hospitali iwe na maji.
All names in Africa have meaning.
Majina yote katika Africa yana maana.
All computers in Kijabe have good internet.
Kompyuta zote katika Kijabe zina internet nzuri.
The entire house needs paint.
Nyumba yote inahitaji rangi.
The entire road from top to bottom will be repaired.
Barabara yote kutoka juu hadi chini itarekebishwa.
It will take a long time for the entire road to be repaired.
Itachukua wakati mrefu kwa barabara yote kurekebishwa.
I always see him all the time outside the bus station.
Mimi humwona wakati wote nje ya kituo cha mabasi.
We used the whole board to repair the store.
Tulitumia ubao wote kurekebisha stoo.
There are trees all over the place.
Kuna miti pote.
The entire place has water.
Pahali pote pana maji.
The entire inside of the hospital has patients.
Hospitalini mwote mna wagonjwa.